MWAMBUSI ASEMA KUREJEA KWA BOSSOU NA NIYONZIMA HAKUTABADILISHA KIKOSI KATIKA MECHI YA KESHO

Wakati mashabiki wa Yanga wakiwa na faraja baada ya kurejea kwa wachezaji wao wa kimataifa Vicent Bosou na Haruna Niyonzima ambao walikua kwenye majukumu ya timu za Taifa,kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi amesema kwamba kurejea kwao hakutakua na mabadiliko katika kikosi cha timu hiyo hasa kuelekea kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Majimaji.

Mwambusi amesema kwamba wachezaji hao hawatacheza kwenye pambano la kesho kutokana kua na matatizo mbalimbali na wengine wakiendelea kua na majeruhi.

"Nikwambia ndugu yangu tulikua tunawategemea sana wachezaji hawa hasa katika mechi ya kesho lkn bahati mbaya hatutawatumia kwa sababu wote wana matatizo" alisema Mwambusi.

Amesema kwamba mchezaji Haruna Niyonzi amerejea akiwa na Maralia huku Vicent Bosou ana matatizo ambayo yatamfanya kukosa pambano hilo sambamba na Mbuyu Twite.

Aidha amesema kwamba kiujumla wachezaji walio salia wako vizuri na kila mmoja ana morali ya kufanya vizuri kwenye pambano hilo litakalopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Hata hivyo amesema kwamba sababu kubwa ambayo imewafanya kutochomoza na ushindi mbele ya Ndanda katika mechi iliyopita ni uchakavu wa uwanja wa Nangwanda,lkn katika pambano la kesho matumaini ya kuibuka na ushindi yapo licha ya kucheza kwenye uwanja wenye nyasi bandia.

No comments