MKWASA ASEMA TANZANIA INA BAHATI MBAYA NA UPANGAJI WA RATIBA
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba mara nyingi Tanzania imekua ikikumbwa na changamoto kubwa ya kupangwa na timu zenye uwezo mkubwa katika ushiriki wa michuano mbalimbali tofauti na nchi za wenzetu kama Uganda na nyingine.
Mkwasa amesema kwamba swala hilo linapelekea timu za Tanzania zishindwe kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ambayo tunapaswa kushiriki kwa kua tunapangwa na timu ambazo zimetuzidi uwezo.
Amesema kua watanzania wanapaswa kufahamu jambo hilo na kuacha kutoa lawama ambazo mara nyingi hua hazina msingi kuhusiana na mwenendo wa timu zetu za Taifa.
Aidha amemtaka Raisi wa TFF,Jamali Malinzi kufanya jitihada za kuzungumza na viongozi wakuu ambao wanahusika na swala zima la upangaji wa ratiba kuliangalia kwa umakini swala hili ambalo mara nyingi hua ni kikwazo kwa nchi yetu.
"Ni vyema siku Raisi wetu wa TFF akiwa kwenye vikao vyao na wakuu hao wa mpira wa miguu ajalibu kuwachomekea jambo hilo hata kwa utani,naamini ujumbe utawafikia wahusika"alisema Mkwasa.
Post a Comment