ANNA KIBIRA AWASHANGAA WALIYOHOJI AFYA YAKE

Aliyewai kua mwenyekiti wa chama cha Netball nchini CHANETA,Anna Kibira amesema kwamba licha ya kuenguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa chama hicho uliomalizika wiki iliyopita kwake hana kinyongo na kitendo hicho.

Kibira ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba ingawa hakuridhishwa na kitendo kilichofanywa na Baraza la michezo Tanzania BMT kushindwa kufuatilia afya yake wakati anaumwa anaamini hilo halitamfanya yeye kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha.

"Ukweli sina kinyongo ispokua nilisikitishwa na habari hizi manaake tangu nimeugua hamna mtu wa baraza aliyesema vipi hali yako kunijulia hali,nimekua nikifanya kazi lakini siku ya siku naambiwa afya yako hauwezi kuendelea kuongoza,nikasema sija budi kukubali nikaambiwa nitakua mshauri wa Netball"alisema Kibira.

Kibira aliondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi wa chama hicho baada ya kamati ya uchaguzi kudai kua afya yake haimruhusu kukiongoza chama hicho.

No comments