MAYANGA ASEMA STARS IPO KAMILI KUWAVAA MALAWI

Kocha wa timu ya Tanzania "Taifa Stars" Salum Mayanga amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi hapo kesho.

Mayanga alisema kwamba dhamira yao kuu ni kushinda kwenye pambano hilo ili kupanda katika viwango vya FIFA na pia mechi hiyo itampa sura ya kutambua nini akifanye katika harakati za kufuzu kwa fainali za Afcon hapo mwakani.

Nae nahodha wa timu hiyo ya Taifa Stars,Mbwana Samata kwa upande wake alisema kwamba wao wamejipanga kupata ushindi kwenye mtanange huo ingawa anaamini mchezo utakua na ushindani wa hali ya juu.

No comments