MASAU BWIRE AMMWAGIA SIFA MWAMUZI ELLY SASSI

Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting,Masau Bwire amemsifu mwamuzi  Elly Sassi kua ni miongoni mwa waamuzi bora ambao anastahili kupongezwa kutokana uwezo wake wa kufuata sheria 17 za soka.

Masau ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba waamuzi wengi wanaochezesha michezo ya ligi kuu wanashindwa kutafasiri vyema sheria 17 jambo ambalo linachangia kudumaza soka letu.

"Nadhani msimu uliopita Elly Sassi ambae alipewa mwamuzi bora hakudanganyiwa, yule ni mwamuzi kijana ambae anajua kazi zake anapokua uwanjani anajua kwamba afanye nini,hata Jonisia Rukya mimi namkubali sana japo wengine wanaona kama hana maamuzi mazuri ni kutokana ni kwamba huenda kwa wakati huo walikosa kile walichokihitaji lakini ni miongoni mwa waamuzi ambao wako vizuri,kina Mwanahamisi Matiko wako waamuzi wazuri kabisa wanaoamua lakini hawa wachache ndio wanaharibu mpira wetu"alisema Masau.

Alisema kwamba mwamuzi Sassi ni miongoni mwa waamuzi ambao wana uwezo mzuri wa kutafasiri vyema sheria 17 kwani kwa mechi ambazo amechezesha hakukuwepo mapungufu makubwa kama ya waamuzi wengine.

Hata hivyo Masau alisema kwamba endapo waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara watatenda haki anaamini ipo siku kikombe cha ligi kuu ya Tanzania bara kitachukuliwa na Ruvu Shooting.

No comments