DONALD NGOMA HATARINI KUWAKOSA KAGERA SUGAR

Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Donald Ngoma leo hii ameshindwa kuungana na wenzake kwa ajili ya kufanya mazoezi ya gym kutokana na majeraha aliyoyapata katika mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Afisa Habari msaidizi wa Yanga,Godlisten Anderson Chicharito ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Dk wa timu Edward Bavu mchezaji huyo italazimika kusubiri saa 24 zijazo kujua kama anaweza kua tayari kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kupigwa 14/10/2017 kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Ngoma alishindwa kuendelea na mchezo wakati wa pambano la ligi kuu ya Tanzania bara lililowakutanisha na Mtibwa Sugar katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam siku ya jumamosi huku timu hizo zikitoshana nguvu baada ya kutofungana.

No comments