MTIBWA SUGAR YATOA USHAURI KWA SIMBA NA YANGA
Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umevitaka vilabu vikubwa vya Simba na Yanga kuacha kasumba ya kutumia gharama kubwa kusajili wachezaji wa nje ya nchi.
Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,Msemaji wa timu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru alisema kwamba vilabu hivyo vinatumia gharama kubwa kusajili wachezaji wa nje ya nchi lakini mwisho wake wanashindwa kuzisaidia vyema timu zao.
Kifaru alisema kwamba timu hizo zinatakiwa kuiga mfumo unaotumiwa na klabu ya Mtibwa Sugar ambao wao wanasajili wachezaji wa ndani ya nchi na pia hawatumii gharama kubwa lakini kwenye ligi hua wanakua na kikosi bora na chenye ushindani.
Alisema mfano mzuri ni mchezo wao wa jana dhidi ya Yanga ambapo amedai kua licha ya Yanga kusheheni wachezaji wengi wa nje ya nchi lakini walishindwa kufurukuta mbele ya kikosi chao na kujikuta wakitoka sale ya kutofungana katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Post a Comment