MARTINEZ AMUONDOA KIKOSINI LUKAKU

Kocha wa timu ya Taifa ya UBELGIJI ROBERTO MARTINEZ amesema kuwa hatakuwa tayari kumjumuisha mshambuliaji wa MANCHESTER UNITED ROMELU LUKAKU kwa kuwa amepata maumivu ya mguu katika enka.

MARTINEZ alisema kuwa LUKAKU pamoja na kuwa mshambuliaji mzuri hatakuwa vizuri watakapopambana na BOSNIA-HERZEGOVINA Jumamosi hii.

Hata hivyo, kocha huyo wa UBELGIJI alisema kuwa LUKAKU anaweza kuwa vizuri na kucheza katika mechi yao ya kufuzu Kombe la Dunia inayofuata dhidi ya SAIPRAS wiki ijayo.

Mshambuliaji huyo wa MAN UNITED ameripotiwa kuendelea vizuri kutokana na vipimo vya madaktari lakini bado hajawekwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa sasa.

LUKAKU tayari amefunga mabao 11 akiwa na Klabu yake ya MANCHESTER UNITED msimu huu. 

No comments