HUMMELS AMPIGIA PANDE JURGEN KLOPP

Mlinzi wa BAYERN MUNICH MATS HUMMELS amesema ana imani na kocha wa LIVERPOOL JURGEN KLOPP kuwa anafaa kuifundisha BAYERN MUNICH baada ya CARLO ANCHELOTTI kufukuzwa.

KLOPP amekuwa akitajwa kuwa huenda angefaa kuwepo BAYERN pamoja na kuwa timu anayoifundisha sasa LIVERPOOL bado inasuasua katika ligi kuu ya ENGLAND.

LIVEPOOL imeanza vizuri msimu katika Ligi kuu ya ENGLAND baada ya kuipiga ARSENAL mabao 4 kwa 0 lakini baada hapo imekuwa tatizo kupata ushindi katika michezo nane iliyocheza.


HUMMELS amekumbuka ushindi mara mbili wa BUNDERS LIGA waliopata akiwa BORUSSIA DORTMUND akiongozwa na JURGEN KLOPP wakati huo.

No comments