ARGENTINA WAWASILISHA OMBI LA KUANDAA KOMBE LA DUNIA

Nchi tatu kutoka bara la Amerika ikiwa ni pamoja Argentina,Uruguay na Paraguay wamewasili maombi ya pamoja kuandaa kombe la dunia mwaka wa 2030.

Kombe la dunia la mwaka 2030 litakuwa maadhimisho ya karne moja tangu mashindano hayo yaanze mwaka 1930.
Marais wa nchi hizi tatu walitangaza mpango huo mjini Buenos Aires siku ya Jumatano Oktoba 4. Hata hivyo zoezi la kumtafua mwandalizi litaanza miaka kadhaa ijayo.
Mkutano wa kwanza wa kuanda ombi hilo la pamoja utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Uruguay imetoa ombi lake hilo wakati inasherehekea miaka 100 kama nchi ya kwanza kabisa kuandaa kombe la dunia.
Wakati huo huo Marekani, Mexico na Canada walitoa ombi la kuanda kombe la dunia mwaka 2026.
Katika kombe la mwaka 2026, jumla ya timu 48, badala ya 32 zitashindana. Hayo ni kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) mapema mweka huu.

No comments