SIMBA YATANGAZA WITO WA AWALI KWA WADHABUNI

Kamati ya Zabuni ya klabu ya Simba leo hii imetangaza kuandaa mwaliko wa awali kwa ajili ya wanachama na taasisi zenye nia na sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni.

Mwenyekiti wa kamati ya Zabuni Thomasi Mihayo alisema kwamba myaraka za mwaliko wa awali ziko tayari hivyo wawekezaji wenye sifa na vigezo wanaweza kuzipata kwa taratibu husika.

Alisema kwamba mwaliko wa kuchukua nyaraka hizo utatangazwa katika vyombo vya Habari kwa muda wa siku 10 ili kuwapatia fursa ya kutosha wazabuni watarajiwa kujiandaa,kukamilisha nyaraka muhimu na kufanya mashauriano muhimu kabla ya kuwasilisha.

Aidha alisema kua tarehe ya mwisho ya kuwasilisha nia ya kushiriki katika mchakato wa kiuwekezaji itakua ni octoba 18/2017 saa 8 alasiri.

Hata hivyo hatua hii itafuatiwa na uchambuzi wa mawasiliano yatakayopokelewa ili kutambua wazabuni watakaokuwa wamekidhi sifa na vigezo.

No comments