BARCELONA KUENDELEA KUCHEZA BILA YA MASHABIKI

Viongozi wa Ligi Kuu ya HISPANIA LA LIGA wamesema BARCELONA itaenda kupambana na ATLETICO MADRID bila ya kuwa na mashabiki wake.


Viongozi wanaosimamia LA LIGA wamesema hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu maalumu.

BARCELONA imesafiri kuelekea mji huo ikiwa Jumapili ya Octoba 14 itakuwa siku ya mapumziko Kimataifa huku mashabiki wa BARCA hawatakuwepo.

Mashambiki wengi wametuma maombi ya kupata tiketi katika mchezo huo lakini ATLETICO haijasambaza tiketi ili mashabiki washuhudie pambano hilo litakalopigwa katika uwanja mpya.

Hata hivyo, imetangazwa kuwa watu 62 ambao walipata tiketi mapema wameelezwa wataruhusiwa kushuhudia mchezo huo.


Imeelezwa hali hiyo imejitokeza baada ya BARCELONA kuifunga LA PALMAS mabao 3 kwa 0 huku uwanja wa CAMP NOU milango ikifungwa kutokana na mvutano mkubwa wa kisiasa uliopo kuhusu uhuru wa eneo la KATALONIA.

No comments