MINGANGE AELEZA UWEPO WAKE KATIKA KIKOSI CHA MSHIKAMANO

Kocha Meja Mstaafu,Abdul Mingange amesema kwamba yeye sio kocha mkuu wa timu ya Mshikamano FC kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu.

Mingange amesema kwamba yeye yuko pale akijitolea baada ya kuombwa na mmiliki wa timu hiyo inayopigania nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

Amesema kwamba kwa kua kazi yake ni kufundisha mpira hakua na tatizo pale alipoombwa kuchukua jukumu hilo na nia yake kwa sasa ni kuona kikosi hicho cha timu ya Mshikamano kinapata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara.

Hata hivyo Mingange alisema kwamba wadau wanapaswa kufahamu kua yeye yuko pale akijitolea kwa kusaidiana na kocha mkuu na dhamira yao kwa pamoja ni kuona mipango yao inafanikiwa.

No comments