SAMATTA AWASILI NCHINI KUUNGANA NA WENZAKE

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine wa Tanzania katika mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Boko Veteran, ulioko Boko - nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa Uhuru,  Jumamosi Oktoba 7, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.

Samata ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Salum Shabani Mayanga.

Stars inajiaanda na mchezo huo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA kwa ajili ya kujiimalisha kabla ya kuanza kushiriki michuano mbalimbali inayoandaliwa na FIFA pamoja na CAF.

No comments