SIMBA HAWANA HOFU NA KAMATI YA HADHI ZA WACHEZAJI

Wakati kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za wachezaji ikitaraji kukaa siku ya jumanne kuyasikiliza malalamiko ya klabu ya Kagera Sugar baada ya kupokwa pointi tatu,mwenyekiti wa tawi la Simba la Mpira Pesa,Ostadhi Masoud amesema kwamba kwa upande wao kama wanachama wa Simba hawana hofu yeyote juu ya jambo hilo.

Masoud alisema kwamba hata kamati ikikaa zaidi ya mara tatu lakini hakutakuwa na mabadiliko yeyote,kwani mchezaji Mohamed Fakh amecheza dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.

Alisema kwamba maamuzi ambayo yametolewa na kamati ya saa 72 ni yenye weledi kwani yamefuata kanuni za uendeshaji wa mpira wa miguu hapa nchini.

Hata hivyo Masoud amewataka wanachama wa klabu ya Simba kuendelea kuwa pamoja kwa kipindi hiki ili kuipa sapoti timu yao na kutimiza azma yao ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu huu.

No comments