NGOMA NA BOSSOU KUWAKOSA TANZANIA PRISONS

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo tayari kupambana na Tanzania Prisons leo hii katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la FA.

Kocha msaidizi wa Yanga,Juma Mwambusi alisema kwamba wachezaji wote wana morali ya kutosha kuelekea kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa 10 kamili jioni kwa saa za hapa nyumbani.

Mwambusi alisema kwamba kuelekea kwenye mechi hiyo watakosa huduma za wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza ambao ni pamoja na Vicent Bossou na Donald Ngoma ambao wote ni majeruhi.

Hata hivyo alisema kwamba licha ya kukosekana kwa wachezaji hao lakini wanaamini watafanya vizuri kwani si mara ya kwanza kwa kikosi hicho kucheza mechi bila ya kuwa na wachezaji tegemeo na wakapata ushindi.

No comments