SHAURI LA KAGERA SUGAR LAPELEKWA CIBER CLAIM

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klbu ya Simba Haji Manara amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo umepata taarifa kutoka kwenye kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji kwamba shauri lao dhidi ya Kagera Suga limepelekwa Ciber claim iliyo chini ya jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Manara alisema kwamba wanaamini maamuzi ya jeshi la Poilisi juu ya uwezo wake katika utendaji kazi lakini wanashangaa kwanini lisipelekwe na TCRA na kwenye vyombo vingine vinavyosimamia na mambo ya IT ambao wana ujuzi wa kujua kama email imefojiwa kama wanataka usawa au kujiridhisha zaidi.

Alisema kwamba uongozi wa Simba umesikitishwa na hatua hiyo na wameitaka kamati husika iwaombe radhi kwa kitendo cha kuwahisi kuwa viongozi wa klabu hiyo wamehusika kufoji email.




No comments