LUDOVIC RUKSA KUICHEZEA AFRIKA LYON

Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji imemuidhinisha mchezaji Venance Ludovic kuendelea kuitumikia klabu ya Afrika Lyon licha ya awali kusimamishwa na TFF baada ya klabu ya Mbao FC kulalamikia usajili wake wakidai kuwa ni mchezaji wao halali.

Katibu mkuu wa TFF,Selestine Mwesigwa alisema kwamba kamati imeamua kuchukua maamuzi hayo baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa TFF na klabu  ya Afrika Lyon walishiriki kuharibu usajili wa mchezaji huyo.

"Kulikuwa na utata fulani kwenye usajili wake na viongozi kadhaa kwa upande wa klabu na shirikisho walishiriki au walichangia kwenye utata huo,kamati imeamua viongozi hao watachukuliwa hatua ambazo zitatangwazwa muda si mrefu kwa maana hiyo kuanzia sasa mchezaji Ludovic ruksa kuchezea Afrika Lyoni lakini Afrika Lyon vilevile kwa jinsi ilivyoshiriki inapata faini ya shiringi laki tano"alisema Mwesigwa.

No comments