CHELSEA NA TOTTENHAM ZAONGOZA KWENYE KIKOSI BORA UINGEREZA

Chelsea na Tottenham zimetawala kikosi cha wachezaji 11 bora wa Ligi ya Premia msimu huu ambacho kimetangazwa na Chama cha Wachezaji wa Soka ya Kulipwa Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na BBC Klabu zote mbili zina wachezaji wanne katika kikosi hicho.
Mabeki Gary Cahill na David Luiz pamoja na viungo wa kati N'Golo Kante na Eden Hazard ndio wachezaji wa Chelsea waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.
Tottenham inawakilishwa na mabeki Kyle Walker na Danny Rose, kiungo wa kati Dele Alli na mshambuliaji Harry Kane.
Mlindalango wa Manchester United David de Gea, Sadio Mane wa Liverpool na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku pia wamo kwenye kikosi hicho.
Kikosi bora cha msimu huu katika Ligi ya Daraja la Pili pia kimetangazwa ambapo wachezaji wanne wa klabu iliyopandishwa daraja hadi Ligi Kuu ya England, Brighton wakiwa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji hao ni golikipa David Stockdale, mabeki Bruno and Lewis Dunk na mchezaji bora wa msimu ligi hiyo, kiungo wa kati Anthony Knockaert.
Newcastle wana wachezaji watatu: beki Jamaal Lascelles, kiungo wa kati Jonjo Shelvey na mshambuliaji Dwight Gayle. Chris Wood wa Leeds, mfungaji mabao bora ambaye ametikisa wavu mara 25 pia ameteuliwa.
Fulham wana wachezaji wawili katika kikosi hicho - beki Ryan Sessegnon na Tom Cairney, ambaye yumo safu ya kati na mchezaji wa Huddersfield Aaron Mooy.

No comments