MTIBWA SUGAR HAKUNA NJAA YA FEDHA KWA WACHEZAJI

Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umesema kwamba ndani ya kikosi cha timu hiyo hakuna mchezaji anaedai mshahara kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu hapa nchini.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar,Tobias Kifaru alisema kwamba Mtibwa Sugar ni miongoni mwa vilabu bora hapa nchini ambavyo huwa makini kwenye swala la ulipaji wa mishahara ya wachezaji kuliko vilabu vingine.

"Hizi taarifa sijui zinatokea wapi maana ndio kwanza nazisikia kwako,Mtibwa Sugar ni kampuni bwana hakuna mchezaji anaelia njaa maana mwisho wa mwezi kila mchezaji anaenda benki kuchukua chake sasa njaa itatokea wapi"alisema Kifaru.

Alisema kwamba kwa sasa wachezaji wote wapo kambini wakijiandaa na maandalizi ya michezo yao ambayo imesalia ili waweze kufanikiwa kuwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments