SAMATA KUIONGOZA GENK KUIKABILI CELTA VIGO

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Mbwana Samata leo hii anataraji kuiongoza timu yake ya Genk kumenyana na Celta Vigo katika mchezo wa Europa League utakaeamua timu itakayofuzu hatua ya nusu fainali.

Genk itaingia kwenye pambano hilo ikiwa na kumbukumbu ya kufugwa kwa jumla ya mabao 3-2 wakiwa ugenini nchini Hispania.

Kwa matokeo hayo itawalazimu Genk kuibuka na ushindi ambao utakuwa tofauti na ule waliopata Celta Vigo wakiwa nyumbani ili kufuzu hatua nyingine.

Mechi hiyo inataraji kupigwa kwenye uwanja wa Luminus Arena nchini Ubelgiji ambapo pambano hilo litachezeshwa na mwamuzi William Collum kutoka Scotland.

Samata ni miongoni mwa washambuliaji tegemeo wa kikosi cha timu ya Genk ambapo leo hii atasimama kama mshambuliaji pekee katika mfumo wa 4-2-3-1.

Hata hivyo Genk ina nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwani inahitaji ushindi wa bao moja tu kuweza kusonga mbele.

No comments