MWESIGWA ASEMA HAYA JUU YA MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI YA TFF

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limesema kwamba kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji leo hii imeshindwa kuketi kujadili malalamiko ya klabu ya Kagera Sugar baada ya kuwepo kwa sababu tofauti.

Katibu mkuu wa TFF,Selestine Mwesigwa amesema kwamba kamati hiyo itakapokamilisha swala hilo basi wataweka wazi wakati wowote kuanzia sasa.

"Naogopa kusema lini swala hilo litakwisha kwa sababu sio mimi ambae naendesha kikao kwa hiyo mwenyekiti ndio anayoweza kusema lini litakwisha swala hilo lakini juhudi ya mwenyekiti na wanakamati kuhakisha kwamba wanamaliza mapema"alisema Mwesigwa.

Hata hivyo Mwesigwa alisema kwamba kwamba yeye hawezi kulumbana na msemaji wa klabu licha ya kuwepo kwa taarifa ya msemaji wa Simba inayopinga kamati ya hadhi za wachezaji kuhusika kwenye shauri la Kagera Sugar.

No comments