AKILIMALI AWASIHI WACHEZAJI WA YANGA WASIWEKE MGOMO

Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga,Ibrahim Akilimali amewataka wachezaji wa timu hiyo hapo kesho wacheze mchezo wa kujituma licha ya klabu hiyo kukabiliwa na ukata mkubwa wa kifedha.

Akilimali alisema kwamba anaamini ukata huo utaisha sio muda mrefu hivyo ni vyema wakaonyesha uungwana wa kuisadia klabu kwa kucheza kwa nguvu zao zote.

Alisema kwamba anaamni baada ya mechi hiyo uongozi utalimazliza tatizo hilo na hata yeye ataenda kuwaona wachezaji kwa ajili ya kuwahamasisha ili wafanye vizuri katika mechi ambazo zimesalia ili timu itwae ubingwa.

No comments