JKT RUVU WAHAHA KUSALIA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kwa sasa kipo jijini Dar es salaam kikiendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na michezo yake mitatu iliyosalia ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Afisa Habari wa JKT Ruvu,Costantine Masanja ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kikosi hicho kinafanya mazoezi kwenye uwanja wake uliopo makao makuu ya JKT,Mlalakuwa chini ya mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden.

Masanja alisema kwamba nguvu kubwa ya mazoezi ni kulenga kupata ushindi kwenye mechi zao tatu zilizosalia ili iepukane na janga la kushuka daraja.

JKT RUVU kwa sasa bado wanaendela kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na alama 23.

No comments