WAZIRI JITU;MSIMAMO WA KWENDA MAHAKAMANI UPO PALEPALE

Katibu mkuu wa tawi la Yanga,Tandale kwa Mtogole,Waziri Jitu amesema kwamba msimamo wake wa kwenda mahakamani siku ya jumanne upo pale pale licha ya kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za wachezaji kuwa na kikao siku hiyo ya jumanne kujadili swala klabu ya Kagera kupokwa pointi tatu.

Jitu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba yeye msimamo wake hautabadilika kwa kuwa kamati ya saa 72 ya TFF imeshindwa kutenda haki kwenye maamuzi ya rufaa ya klabu ya Simba,baada ya kamati hiyo kuipa pointi tatu na magoli matatu kwa kitendo cha klabu ya Kagera Sugar kumchezesha mchezji mwenye kadi tatu za njano.

Alisema kwamba kwa sasa TFF inaendeshwa na matakwa ya mtu mmoja na ndio maana maamuzi yanayotolewa hayana usawa kwa baadhi ya vilabu.

"Ndugu mwandishi ebu nikuulize hivi kamati ya saa 72 na kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za wachezaji ipi yenye uhalali wa kusimamia ligi?mimi naona hilo wanalotaka kulifanya halitakuwa na mabadiliko yeyote,wewe njoo jumanne mahakama ya Kisutu saa mbili asubuhi utanikuta nikifungua kesi,kama noma na iwe noma ni bora tufungiwe kucheza soka na FIFA"alisema Jitu.

Kamati ya saa 72 ya TFF iliipoka pointi tatu na magoli matatu klabu ya Kagera  Sugar baada ya kamati hiyo kubaini kuwa timu hiyo ilimchezesha mchezaji Mohamed Fakh akiwa na kadi tatu za njano,ambapo maamuzi hayo yamepingwa vikali na viongozi wa Kagera Sugar na uongozi wa klabu ya Yanga.

No comments