WACHEZAJI NA VIONGOZI WA YANGA WAACHWA NA NDEGE

Kundi la pili la wachezaji na viongozi wa Yanga waliokuwa waondoke Algeria leo hii,wameachwa na ndege ya Uturuki baada ya kuchelewa kufika uwanja wa ndege.

Taarifa ambazo zimepatikana zinaeleza kuwa sasa wachezaji hao watarejea siku ya jumatano na shirika la ndege la Uturuki taksh Airlines ambalo ni shirikia hilohilo lililowataka kuwachukua leo hii.

Kundi hilo la pili linaongozwa na katibu wa timu hiyo Charse Boniphace Mkwasa ambae inasemekana hapo jana alikuwa wa kwanza kuwahamasisha wachezaji wazingitie muda wa kuwai ndege kwa ajili ya kurejea hapa nchini.

Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika na timu ya MC Alger ya Algeria baada ya kukubali kufungwa kwa jumla ya bao 4-0.

Hata hivyo kuna taarifa kuwa kundi hilo la pili la wachezaji ambao walichelewa kuwasili nchini Algeria wamelalamika kuwa na uchovu wa safari kwani walifika siku ya ijumaa na kucheza mechi siku ya jumamosi.

MWANDIKE.BLOGSPOT inaendelea kufuatilia swala hilo ili kubaini ni sababu zipi ambazo zimepelekea kwa wachezaji hao pamojana viongozi kuchelewa ndege kwa wakati wa muafaka.

No comments