TFF;TUMERATIBU SAFARI YA YANGA LAKINI SIO KUTOA PESA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limekili kuisaidia klabu ya Yanga kupata ndege kwa siku ya leo ili wachezaji pamoja na viongozi warejee hapa nyumbani.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba wao TFF wamehusika katika swala la kuratibu ndege ya haraka tofauti na waliyotafuta wao iliyotaraji kuwarejeshe siku ya jumamtano.

Lucas alisema kwamba kwenye maswala ya fedha klabu ndio imehusika na wala sio TFF kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu.

Hata hivyo amedai kuwa ni vyema watanzania wakafahamu kuwa linapokuja swala la uwakilishi wa kimataifa kwa timu za vilabu,TFF ina jukumu la kusimamia vilabu vyake, hivyo kwa hilo ambalo wamelifanya ni sahihi baada ya kuona wana uwezo wa kulitatua swala hilo.

No comments