ARSENAL KUMENYANA NA MIDDLESBROUGH

Leo Arsenal wanacheza dhidi ya Middlesbrough ambao wataongezewa nguvu na kurejea kwa Captain George Friend ambaye anatokea katika majeruhi ya kifundo cha mguu.
Gaston Ramirez atakuwepo pia baada ya kutokea katika maumivu ya enka.
Arsenal wanaweza kuwa naye tena Captain Laurent Koscielny ambaye naye alikuwa majeruhi kwenye pambano hilo litakalopigwa mishale ya saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Pambano hilo litakalopigwa kwenye uwanja wa Riverside litaachezeshwa na mwamuzi Anthony Taylor.
Arsenal kwa sasa ipo katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England ikiwa na alama 54 baada ya kucheza miechi 30.
Chelsea licha ya kufungwa kwa jumla ya mabao 2-0 na Manchester United hapo jana lakini wanaendelea kuongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa alama 75 baada ya kucheza mechi 32 wakifuatiwa na Tottenham Hotspur wenye alama 71 nayo ikicheza michezo 32.

No comments