MOHAMED HUSSEIN ATAKA HAKI ITENDEKE KWENYE SHAURI LAO

Katibu mkuu wa klabu ya Kagera Sugar,Mohemed Hussein amesema kwamba kwa upande wao hawana hofu yeyote juu ya maamuzi yatakayotolewa leo hii na kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji juu ya malalamiko yao ya kupinga kupokwa pointi tatu na kamati ya saa 72.

Hussein alisema kwamba wao wanaamini wana haki ya kurejeshewa pointi zao tatu ambazo walizipata uwanjani kwani mchezaji Mohemed Fakh hakupewa kadi tatu za njano kama inavyoelezwa.

Alisema kwamba licha ya kamati hiyo kushindwa kutoa maamuzi siku ya jana baada ya kukosekana kwa baadhi ya ushahidi na nyalaka lakini wao hawana wasiwasi wowote ispokuwa wanachotaka haki itendeke.

"Sisi tunasema waahirishe hata mwezi lakini tupate haki yetu hatuna mashaka na kuahirishwa, kwa sasa ukiangalia katika hili wenzetu ndio wana presha kubwa za hizo pointi kuliko sisi kiukweli na sisi tunaziitaji zaidi kuliko wao lakini wao wana presha nikiseme hivyo unajua kwa nini wana presha,timu ambayo takribani ambayo haijabeba kombe takribani miaka mitano wanategemea kupitia hapa lazima watakuwa na presha lakini lazima tuwape nafasi viongozi wa kamati"alisema Mohamed.

Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji inataraji kutoa maamuzi juu ya shauri hilo leo hii baada ya kupitia ushahidi na nyalaka ambazo zilikosekana kwa siku ya jana.

No comments