KAGERA SUGAR KUPOKWA POINTI ZA SIMBA

Uongozi wa klabu ya Simba umewasilisha rufaa kwa waendeshaji wa bodi ya ligi wakitaka Kagera Sugar ipokwe pointi tatu wakidai kuwa timu hiyo imemtumia mchezaji Mohamed Fakhi mwenye kadi tatu za njano.

Kamati ya masaa 72 ya TFF leo hii inataraji kukaa na kupitia rufaa mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kamati hiyo ikiwemo swala hilo la Simba.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Kagera Sugar kupitia kwa kocha mkuu  Meck Mexme amesema kwamba mchezaji huyo hana kadi tatu za njano kama inavyodaiwa na klabu ya Simba.

Mexme amesema kwamba yeye na uongozi wake una kumbukumbu ya kadi kwa kila mchezaji wa Kagera Sugar hivyo wanachotaka kufanya Simba kama kutaka kujihangaisha.

Aidha ameihatadharisha bodi ya ligi kuwa makini na jambo hilo,kwani wasije wakafanya mambo yao kiushabiki pasipo kufuata misingi na taratibu za uendeshaji wa ligi,kwani wao wana data kamili na hawataweza kukubali kupokwa pointi.

Kagera Sugar inaweza kupokwa pointi tatu endapo bodi ya ligi itabaini kuwa ni kweli mchezaji huyo alicheza akiwa na kadi tatu za njano,kwa mujibu wa kanuni ya uendeshaji wa ligi.

Katika hatua nyingine kwa sasa kuna taarifa imezagaa kwenye mitandao tofauti ikieleza namna ya kadi alizopewa Mohamed Fakhi.

SOMA HAPO CHINI TAARIFA HIYO.


KADI TATU ZA NJANO ALIZOPATA FAKHI MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR
1. Mchezo namba 122 uliopigwa Sokoine tarehe 17 December dhidi ya Mbeya City.

2. Mchezo namba 165 uwanja wa Kaitaba mchezo dhidi ya African Lyon . Ulipigwa tarehe 18 January.
3. Mchezo namba 190 uwanja wa Kaitaba tarehe 4 March , mechi dhidi ya Majimaji.

Mechi hizi ndizo ambazo zimewafanya Simba SC kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa kumchezesha mlinzi wao Mohamedi Fakhi katika mechi ya April 2, 2017 Kaitaba ambapo Simba alifungwa goli 2-1.

Kama madai haya yatakuwa kweli kwa ushahidi wa mechi hizo tatu , ina maana Simba watapewa alama tatu za mchezo huo waliopoteza.

No comments