WENGER AWASIFU MASHABIKI WA ARSENAL

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wazuri sana wakati wa mechi dhidi ya Manchester City ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 uwanjani Emirates.
Amesema hayo licha ya kwamba bado wapo mashabiki walioandamana kumpinga wakati wa mechi hiyo ya Jumapili.
Wenger, ambaye anakabiliwa na shinikisho baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni amekuwa akitakiwa na baadhi ya mashabiki ajiuzulu.
"Lazima niseme kwamba, licha ya yote yaliyofanywa na baadhi ya mashabiki, mashabiki wetu walikuwa wazuri sana leo," alisema Mfaransa huyo baada ya mechi.
Arsenal, ambao wameshuka hadi nafasi ya sita kwenye Jedwali, walitoka nyuma mara mbili kulazimisha sare hiyo dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola.
"Katika nyakati ngumu sana, tukiwa 1-0 chini na 2-1 chini, wangetugeuka lakini nafikiri walikuwa wazuri sana na walituwezesha kupitia vipindi hivyo vigumu."
Mabao kutoka kwa Theo Walcott na Shkodran Mustafi cyalisaidia Arsenal kukomboa mabao kutoka kwa Leroy Sane na Sergio Aguero.
Wenger anaamini matokeo katika mechi hiyo yatawarejeshea Arsenal imani na kuwawezesha kurejelea ushindi wao kama zamani.
Mkataba wa Wenger unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Ameahidiwa mkataba wa miaka miwili na alsiema mnamo Machi 18 kwamba atatangaza uamuzi kuhusu mustakabali wake hivi karibuni.
Kipa wa zamani wa ,Bob Wilson aliambia BBC kwamba Wenger anafaa kutangaza mustakabali wake "kwa maslahi ya klabu".
Lakini Wenger Jumapili alisema: "Nimeonesha uzalendo na nimeendelea kujitolea. Sijui nitakuwa hapa muda mgani lakini naipenda klabu hii na nitafanya lililo njema Nitafanya hilo karibuni, msiwe na wasiwasi."
Arsenal wamo namabri sita katika Ligi ya Premia kwa sasa, alama saba nyuma ya Manchester City walio nambari nne.
Gunners watakutana na West Ham nyumbani Jumatano kisha wasafiri Crystal Palace Jumatatu.

No comments