JKT RUVU WAENDELEA KUWEPO MKOANI SHINYANGA

Kikosi cha timu ya soka ya JKT Ruvu bado kinaendelea kuwepo mkoani Shinyanga kabla ya kuelekea mkoani Kagera kujiwinda na pambano lao dhidi ya Kagera Sugar hapo siku ya jumamosi.

Afisa Habari wa JKT RUVU,Costantino Masanja amesema kwamba,baada ya kupata alama moja kwenye pambano lao dhidi ya Mwadui,wachezaji wa timu hiyo kila mmoja amepata hamasa kubwa ya kuisadia timu yake.

Masanja amesema kwamba licha ya kuwepo katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi lakini bado wana imani kubwa ya kusalia ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

No comments