MAJIMAJI KUCHEZA NA AFRIKA LYON BILA YA NAHODHA

Kocha wa timu ya Majimaji ya Mkoani Ruvuma,Kally Ongala amesema kwamba licha ya kukosekana kwa nahodha wake katika mchezo ujao dhidi ya Majimaji anaamini kikosi cha timu hiyo kitafanya vizuri.

Ongalah alisema kwamba nahodha wa timu hiyo alipewa kadi nyekundu katika pambano lao lililopita dhidi ya Toto Africans,hivyo atakosekana kwenye mechi yao ya jumamosi dhidi ya Afrika Lyoni.

Alisema kwamba anaamini yule atakaechukua jukumu lake atafanya vizuri,kwani dhamira yao ni kuona wanasalia ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

No comments