SIMBA WAWASILI MWANZA KUWAVAA MBAO FC

Baada ya kupoteza pambano lao dhidi ya Kagera Sugar kwa kukubali kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1,kikosi cha Simba kimeshawasili mkoani Mwanza kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mbao FC.

Mratibu wa Simba,Abasi Ally alisema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mechi zote ambazo zimesalia ikwemo dhidi ya Mbao FC na nia yao kuona wanaibuka na ushindi kwenye mechi zote.

Abasi alisema kwamba kwa sasa bado wana ndoto za kuwa mabingwa wa ligi kuu,kwani mechi bado zimesalia na lolote linaweza kutokea licha ya kuwa nyuma kwa pointi moja na anaeongoza ligi.

Hata hivyo alisema kwamba anaamini mashabiki wa Simba bado wana imani na kikosi chao,hivyo kwa sasa ni vyema wakaelekeza nguvu zao kwenye mechi zote za ligi ambazo zimesalia.

No comments