IDD CHECHE AMKUMBUKA JOHN BOKO

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Azam FC,Idd Cheche alisema kwamba kikosi chake kimeshindwa kuibuka na ushindi katika pambano lao jana dhidi ya Yanga kutokana na kukosekana kwa mshambuliaji wao  John Boko.

Cheche alisema kwamba wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi za wazi lakini kulikuwa hakuna mshambuliaji aliyezitumia vizuri nafasi hizo licha ya kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa.

Boko alishindwa kucheza pambano hilo kutokana na kukabiliwa na majeruhi ambapo taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo atakuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja kwa mujibu wa daktari.

Azam FC,hapo jana walikubali kufungwa kwa bao 1-0 mbele ya Yanga katika pambano la ligi kuu ya Tanzania bara lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments