TIMU YA TENISI KUSHIRIKI MICHUANO YA DUNIA

Timu ya taifa ya Tenisi ya watu wenye ulemavu inahitaji msada mkubwa wa fedha na vifaa ili kuhakikisha wanashiriki vyema mashindano ya dunia ya BNP Paribas World Team yatakayofanyika nchini Itali kuanzia tarehe moja ya mwezi wa tano hadi tarehe saba mwaka huu.

Mwenyekiti wa chama cha Tenisi Tanzania,Dennis Makoi alisema kwamba kwa sasa washiriki wanaendelea vyema na maandalizi lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa ambavyo vitawawezesha kushiriki vyema mashindano hayo.

Makoi alisema kwamba kiujumla hali maandalizi kwa upande yako vizuri kwani wachezaji wanaendelea vyema na mazoezi ili kuweza kufanikisha wanafanya vyema kwenye mashindano kwa kuipeperusha vyema bendera ya Taifa na Afrika kwa ujumla.

Nae kocha mkuu wa timu hiyo Riziki Salum alisema kwamba kikosi chake kinataraji kuanza safari siku ya tarehe 29 ya mwezi huu ikiwa na jumla ya wachezaji 4.

Riziki alisema kwamba bado msafara huo unakabiliwa na  changamoto kubwa katika upande wa tiketi,hivyo ni vyema wadau na makampuni kujitokeza kuisaidia timu hiyo ya Taifa ya mchezo wa Tenisi kwa watu wenye ulemavu.

No comments