MWAMBUSI AMJIA JUU JONESIA RUKYAA

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga Juma Mwambusi alisema kwamba hakuridhishwa na maamuzi ya mwamuzi Jonisia Rukyaa kutoka mkoani Kagera, kwa kitendo chake cha kuongeza zaidi ya dakika 9 katika pambano lao ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Mwambusi alisema kwamba ameshangazwa na kitendo hicho cha mwamuzi kuongeza dakika 4 zaidi ili halia ziliongezwa dakika 5 kwenye pambano hilo lililoisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0,goli lililofungwa na mchezaji Obrey Chirwa.

Alisema kwamba yeye hawezi kuzungumzia juu ya uchezeshaji wake kwenye pambano hilo kwa kuwa hana uwelewa wa jambo hilo lakini ameshangazwa na kitendo cha kuongeza dakika nyingi zaidi.

No comments