TANZANIA YAPANDA KWA NAFASI 22 FIFA

Tanzania imependa kwa nafasi 22 kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kutoka kwenye nafasi ya 157 hadi 135.

Kupanda kwa Tanzania kumechagizwa na kufanya vizuri kwenye mechi mbili za kirafiki zilizochezwa kwenye kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana kabla ya kupata ushindi mwingine wa mabao 2-1 mbele ya Burundi.

Uganda inaendelea kuongaza katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wakiwa nafasai ya 72 wakifuatiwa na Kenya iliyopo kwenye nafasi ya 78 huku Rwanda ikikamata nafasi ya 117.

Brazili ndio nchi ya kwanza inayoongoza kwenye viwango hivyo wakifuatiwa na Argentina huku nafsi ya tatu ikishikiliwa na Germany.

Kwa Afrika Misri ndio wanaongoza katika viwango hivyo,Senegal imeshika nafasi ya pili na ya tatu ni Cameroon.

No comments