JESHI LA POLISI LAWAKEMEA MASHABIKI WA MC ALGER

Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha mashabiki wa timu ya Yanga na Mc Alger kuacha tabia ya kuwasha miale ya moto uwanjani,kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa.

Kamishina wa kanda maalumu ya Dar es salaam,Simon Siro alisema kwamba katika mchezo wa leo wa kombe la shirikisho barani Afrika hawatakubali kuona jambo hilo linatokea.

Alisema kwamba kama ilitokea huko nyuma labda jeshi hilo halikubaini tukio hilo,lakini kwa leo wameweka askari wa kutosha ambao watakaa kila pembezoni mwa uwanja.

No comments