YANGA YAWEKA BAYANA MJADALA WA KOCHA STEWART

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga SC,Charles Boniface Mkwasa , mchana wa leo amezingumza na waandishi wa habari katika mkutano mfupi ofisi kwake katika kutoa ufafanuzi wa uzushi wa Yanga kutafuta kocha mpya pia ujio wa timu ya MC Alger kwa mchezo wa kombe la shirikisho.

Kabla ya maelezo juu ya uzushi wa kocha mpya na ujio wa MC Alger , katibu huyo alitoa bei za viingilio vya mechi yao na waarabu hao jumamosi hii uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

BEI ZA TIKETI

1.Mzunguko 5000
2. VIP B & C  20000
3. VIP A  30000

UJIO WA MC ALGER

MC Alger watafika siku ya alhamisi saa tatu na nusu usiku na ndege maalum ya kukodi moja kwa moja toka Algeria.

Kuhusu Stewart Hall kocha wa zamani wa Azam FC kufanya mazungumzo na klabu ya Yanga Mkwasa amesema kwamba ni uzushi wa mitandaoni na watu wasio na nia njema kwa klabu yetu.

Alisema kwamba Yanga haina mpango wowote na kocha huyo wala kocha yoyote kwa sasa ambapo amedai kuwa hizo ni chokochoko na wanazipinga vikali.

" timu yetu kwa sasa inaongoza ligi na tupo katika njia nzuri za kuutetea ubingwa wetu,hawa wanaoleta maneno ya uzushi hawana nia njema na klabu , wanataka watu waache kufanya kazi ili malengo yao yatimie.

 Klabu haipo katika mpango ambao moja kwa moja ni hasara kwa klabu kuanza kulipa fidia na kupoteza malengo yake .

Mkwasa pia amesisitiza kuwaomba watanzania na wapenzi wa soka kiujumla kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu uwanjani dhidi ya waarabu hao ili kushinda mchezo huo wa mwisho wa juma.

" tunahitaji kushinda hapa nyumbani ili kupunguza ugumu wa mechi ya ugenini , hivyo sapoti yenu itakuwa ni msingi mzuri wa morali kwa vijana"alisema Mkwasa.

No comments