YONDANI NA TAMBWE KUWAKOSA MC ALGER

Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu timu ya soka ya Yanga imesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Mc Alger ya Algeria hapo kesho katika mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Kocha msaidizi wa Yanga,Juma Mwambusi alisema kwamba leo hii wachezaji wake wamemaliza vizuri mazoezi na kila mmoja ana hamasa ya kufanya vyema kwenye pambano hilo linalotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mwambusi alisema kwamba kuelekea kwenye pambano hilo wanataraji kukosa huduma za mchezji wao Cavin Yondani baada ya kuumia leo hii wakati wa mazoezi ya asubuhi.


No comments