SAMATA AENDELEZA WIMBI LA KUZIFUMANIA NYAVU

Mshambuliaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Mbwana Samata ameendeleza wimbi lake la kuzifumania nyavu baada ya hapo jana kuisaidia timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya timu ya Lokeren katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza UEFA Europa league msimu ujao.

Katika mchezo huo wa kundi B,Samata aliifungia Genk bao kunako dakika ya  72 ya mchezo ikiwa ni bao la pili la kwanza likifungwa na Bryan Heynen kabla ya Boetius na Naranjo kuhitimisha ushindi huo wa mabao 4-0.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars juma lililopita aliisaidia Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki huku yeye akifunga magoli yote mawili.

No comments