SIMBA WAKOMBOA NYASI BANDIA

Uongozi wa klabu ya wekundu wa msimbazi Simba umesema kwamba umemalizana na mamlaka ya forodha yaTRA juu ya malipo ya nyasi bandia ambazo hivi karibuni zilitangazwa kupigwa mnada na kamupuni ya madalali majembe kutokana na kukaa kwa muda mrefu bandarini pasipo kulipiwa kodi.

Makam wa Rais wa klabu ya wekundu wa msimbazi Simba Geofrey Nyange Kaburu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba wamefanikiwa  kulipa deni lote ambalao walikuwa wanadaiwa na sasa wako katika hatua za mwisho za kukamilisha nyasi hizo kutoka bandarini.

Kaburu alisema kwamba yeye pamoja na uongozi mzimz wamefuraji sana kukamilisha malipo hayo na zitakapotoka tu watazipeleka moja kwa moja kuanza ujenzi wa uwanja wao wa mazoezi kwa ajili ya msimu ujao.

No comments