AFRIKA LYON YAIFUATA MAJIMAJI KWA NGUVU MOJA

Kikosi cha timu ya Afrika Lyon hapo kesho kinataraji kuelekea mkoani Ruvuma kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Majimaji.

Kocha mkuu wa timu hiyo Charles Otieno ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kwa upande wao wamejiandaa vizuri na leo hii wamemaliza mazoezi vizuri,hivyo kilichosalia ni kuanza safari hapo kesho.

Otieno alisema kwamba anaamini mechi itakuwa ngumu kutokana na nafasi iliyopo kwa timu hizo lakini kwake amejipanga kuhakikisha anaibuka na ushindi.

Aidha alisema kwamba katika msafara wa kesho hawataambana na mchezaji wao mmoja Hawazi kutokana na kukabiliwa na adhabu ya kadi tatu za njano.

No comments