MBEYA CITY, MTIBWA SUGAR UWANJANI KESHO VPL

Ligi Kuu ya Vodacom  Tanzania Bara, kesho Jumatano Aprili 5, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo huo unataraji kuwa na ushindani kwa pande zote kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu ili ijiweke kwenye mazingira mazuri kwenye nafasi za juu katika msimamo wa ligi.


Wakati huo huo Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.

Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.

No comments