KAMATI YA RUFANI YA TFF YAMUENGUA KUWAYAWAYA KUWANIA UCHAGUZI WA DOREFA



Kamati ya rufani ya TFF,ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo wakili Julias Lugaziya imetupilia mbali shauri la Stivin Kuwayawaya aliyekua amekata rufaa juu ya kuenguliwa kwenye mchakato wa kuwania uongozi wa chama cha soka mkoani wa Dodoma [DOREFA]

Akiongea na Mwandike.blogsport,mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wakili Lugaziya amesema kwamba baada ya kupokea shauri hilo kamati imekaa na kupitia vielelezo vyote ikiwemo kusikiliza hoja kwa upande wa mrufani pamoja na mkata rufaa na kubaini kua muomba rufaa hakustahili kuwemo kwenye uchaguzi wa chama hicho baada ya kugundua kutokua na sifa za kugombea ikiwemo kutowasilisha usibitisho wa uraia wake

Katika hatua nyingine mkata rufaa wa shauri hilo Stivin Kuwayawaya amesema kwamba kamati hiyo haikutenda haki juu ya maamuzi hayo kwani kuna mambo muhimu aliyawasilisha lkn hayakuzungumzwa na kamati hiyo

Akiongea na ABM RADIO amesema kwamba yeye anakubaliana na maamuzi hyo lkn anaamini kuna baadhi ya watu ambao baadhi yao wamo ndani ya TFF,wamehusika kumuondoa kwenye uchaguzi hou

Aidha ameshangazwa na kipengele ambacho kamati imeona hana sifa za kua kwenye uchaguzi wa chama hicho kwa sababu mgombea hana uzoefu wa miaka mitano ilihali yeye amekua katika mfumo wa soka kwa muda mrefu na amewai kuteuliwa na chama cha mpira wa miguu hapa nchini mwaka 1994 kusafiri na timu ya Taifa ya Tanzania kwenda Kenya kushiriki michuano inayoandaliwa na CECAFA kwa sasa na timu hiyo imefanikiwa kurejea na kombe

No comments