KISA JEZI MASHABIKI WA SIMBA WASUSA KUSHANGILIA


Wakati timu ya soka ya Yanga ikitarji kushuka dimbani kumenyana na Medeama ya nchin Ghana katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika,baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba wamesema kwamba kueleka kwenye pambano hilo wao hawataweza kuishangilia timu ya Medeama kwa sababu timu hiyo inatumia jezi zenye rangi inayofanana na za mahasimu wao wa jadi

Akiongea na Mwandike.blogsport,mwenyekiti wa tawi la Simba la Mpira Pesa Ostadhi Masoud amesema kwamba sababu kubwa ambayo imewafanya kutoishangilia Medeama ni jezi ambazo wanavaa kufana zaidi na jezi za Yanga hivyo kutokana na jambo hilo haitakua vyema kuwapa ushirikiano kwenye pambano hilo

Amesema kwamba katika ushabiki wa watani wa jadi swala wa Simba na Yanga lipo katika rangi hivyo awali walikua wanazipa sapoti timu nyingine kama TP,Mazembe na nyinginezo kwa kua wamekua wakitumia jezi ambazo hazilingani na za Yanga

No comments