TANZANIA YAPANDA KATIKA VIWANGO VYA UBORA WA FIFA
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limetoa orodha ya
viwango vya soka duniani kwa mwezi Julai huku Tanzania ikipanda kwa nafasi
13 licha ya kutocheza mchezo wowote
tangu ilipofungwa na Misri tarehe 4 Juni.
Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 136 mwezi uliopita hadi
nafasi ya 123 dunani huku ikishika nafasi ya 33 barani Afrika.
Kwa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni taifa pekee la
ukanda wa CECAFA lililosalia katika mbio za kuwania kufuzu Kombe la Dunia
imeendelea kwa kupanda nafasi 3 na sasa kushika nafasi ya 14 na 69 duniani.
Afrika nchi ya Algeria imeendelea kuongoza huku ikiahika
nafasi ya 32 duniani, Ivory Coast
inashika nafasi ya 35 na Ghana ikiwa
nafasi ya tatu na nafasi ya 36 duniani.
Kwa dunia, Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza
ikifuatiwa na Ubelgiji na Colombia katika nafasi ya pili na tatu.
Post a Comment