JULIO ASEMA YEYE ALISTAHILI KUWEMO KATIKA KUWANIA TUZO YA KOCHA BORA WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


Kocha mkuu wa timu ya Mwadui,Jamhuri Kiweru Julio ametoa lawama zake kwa kamati inayohusika na utoaji wa tuzo za washindi wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara kwa kusema kwamba hawakutenda haki kwa baadhi ya uteuzi wa wachezaji na makocha kuelekea kwenye kuwapata washindi hao

Julio amesema kwamba anashangaa mtu kama yeye kutowepo kwenye tuzo ya kuwania kocha bora ili hali ameweza kuisaidia vyema timu yake ya Mwadui na kufanikiwa kufika hadi nusu fainali ya michuano ya kombe la FA na kuonyesha ushindani wa kutosha katika mechi mbalimbali za mashindano pasipo kua na hata mchezaji wa kigeni

Aidha ameshangazwa kutokuwepo mchezaji wa Azam,Shomari Kapombe kwenye tuzo ya mchezaji bora licha ya kua mchezaji ambae ametoa mchango mkubwa katika timu yake iliyomaliza kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments