AZAM WAPANGA KUSAJILI WACHEZAJI 4 KUTOKA NJE YA NCHI
Wakati dirisha la usajili wa wachezaji likitarajiwa kufungwa,Mtendaji mkuu wa timu ya Azam,Saad Kawemba amesema kwamba
msimu huu uongozi wa klabu hiyo umepanga kufanya usajili wa wachezaji wanne
kutoka nje ya nchi na hawana mpango wowote wa kusajili mchezaji wa hapa
nyumbani kwa kua wachezaji waliopo ndani ya klabu hiyo ni bora kuliko wachezaji wote wa hapa nyumbani
Akiongea na Mwandike.blogsport Kawemba amesema kwamba kwa sasa wamefanikiwa kupandisha
wachezaji wanne wa timu ya vijana ya Azam ambao hawa wataungana na wachezaji
wanne wapya watakaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania
bara
Kawemba amesema kwamba msimu ujao wanatarajiwa kuwa na jumla
ya wachezaji 44 ambapo wachezaji 22 watakua kikosi cha kwanza na 22 ni
wachezaji wa timu ya vijana
Post a Comment